Select Menu

News

News

Music

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.

Movie

Gossip

Life Style

Sports

Health

Documentary

Video

» » » » » » mahiri wa upasuaji kubadili sura Korea Kusini wawaletea wateja shida ya utambulisho


Mwananchi Kweli 1:28 AM 0


Korea Kusini hivi sasa inasifika na kuaminika katika teknolojia ya upasuaji wa kubadili sura (plastic surgery) kiasi cha kuwavuta raia wa nchi jirani kuifuata huduma hiyo.
Kwa mujibu wa mitandao ya Korea Kusini, Onboa na Munhwa, upasuaji mwingine hufanyika na kubadilisha kabisa sura ya mteja kiasi cha kupoteza utambulisho wake kama alivyokuwa anaonekana kwenye picha ya passport aliyotumia kuingia nchini humo.
Kutokana na tatizo hilo, hospitali zinazotoa huduma hiyo zimeanza kuwapa wateja wao hasa wageni vyeti maalum vya utambulisho mpya ambavyo vinakuwa na jina la mteja na namba ya passport yake, jina la hospitali aliyofanyiwa upasuaji na muda alioutumia kuitembelea nchi ya hiyo.
Imerepotiwa kuwa mwaka 2009, wanawake 23 wa China walipata usumbufu mkubwa wakati wanataka kutoka Korea Kusini baada ya kufanyiwa upasuaji kwa kuwa ilikuwa vigumu kuwatambua.



«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply