Select Menu

News

News

Music

Theme images by konradlew. Powered by Blogger.

Movie

Gossip

Life Style

Sports

Health

Documentary

Video

» » KUHUSU MLIPUKO ULIOTOKEA BAR YA NIGHT PARK ARUSHA!!! HIZI HAPA PICHA NYINGINE 6 ZA ENEO MLIPUKO ULIPOTOKEA.


Mwananchi Kweli 2:32 AM 0

Picha hapo juu ikiwa inaonyesha Bar ambayo mlipuko huo ulitokea. (picha zote na Rajab Makenda n4t Arusha)
Na Rajab,Arusha.Mlipuko mkubwa ulitokea jana majira ya saa 1.30 usiku katika baa maarufu ya Arusha night park iliyopo eneo la Mianzini mjini Arusha. Taarifa tulizo zipata hapa eneo la tukio zinaeleza kuwa mlipuko huo unatokana na bomu lililotegwa katika eneo la bar hiyo na kujeruhi watu zaidi ya 20 waliokuwa wakiangalia mchezo wampira wa miguu ligi kuu ya England kati ya Chelsea na Swansea.


Majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Selian na Mount Meru. Mashuhuda wanaeleza kuwa kuna baadhi ya majeruhi wamekatika viungo kama miguu na vidole. Bado hatuja pata Habari za uhakika kwani mda huu ndio mkuu wa mkoa wa Arusha ameingia pamoja na watu wa vipimo vya mabom na tayari wamesha anza kazi ya kupima ili kujua aina ya bom na lilipo tengenezewa. Baada ya vipimo Mkuu wa jeshi lapolisi Arusha atatoa maelezo ambayo tutawawekea hapa www.news4timeblog.com. Tunakuomba uendelee kutembelea tutakujuza zaidi.


Hapo chini ni picha za eneo la tukio.


Askari wa Mabom wakiwa wanalinda eneo lililo athirika na mlipuko huo likiwa limezungushiwa utepe wa Police line.

Hapa ni eneo la bar ya jirani na Night park ambalo pia liko chini ya ulinzi.

Hapo kwa ndani ni uharibifu uliotokea kutokana na bom hilo.

Viti na meza vikiwa vimevunjikavunjika kutokana na mlipuko huo.


Hawa ni baadhi ya watu waliofika eneo hili asubuhi ya leo wengine wakiwa ni moja ya walio nusurika katika Mlipuko huo.

Endelea kutembelea news4timeblog.com Tutakuwa tunawaletea kinachoendelea.

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments

Leave a Reply